IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mauritania yafanya mashindano ya kuchagua wawakilishi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

17:05 - February 14, 2024
Habari ID: 3478348
IQNA - Mashindano ya nchi nzima ya Qur'ani yanaendelea nchini Mauritania ambayo yanalenga kuchagua wawakilishi wa nchi hiyo ya Kiafrika kwa ajili ya mashindano yajayo ya kimataifa ya Qur'ani.

Takriban washiriki 500, wakiwemo wanawake 90, wameshiriki katika shindano hilo lililoanza Jumatatu.

Mashindano hayo yameandaliwa na wizara ya masuala ya Kiislamu nchini humo na yanalenga kuchagua wawakilishi wa Mauritania katika mashindano yatakayofanyika katika nchi tofauti kama vile Malaysia, UAE, Kenya, Kuwait, n.k.

Akihutubia katika hafla ya uzinduzi, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania Dah Ould Sidi Ould Amar alisifu ushiriki mkubwa wa makari na wahifadhi katika toleo hili la tukio.

Alisema mashindano hayo yatakuwa kama nyongeza ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka. Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu. Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika.

3487182

captcha