Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, Dawah na Mwongozo imekamilisha maandalizi ya mashindano hayo ya kwanza ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Sunnah za Mtume (SAW) ambayo yatafanyika kufanyika kuanzia tarehe 15 hadi 19 Oktoba.
Mashindano hayo yanafanyika kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Elimu Asilia nchini Mauritania, na yanapangwa kufanyika kila mwaka katika nchi za Afrika Magharibi.
Jumla ya washiriki 136 kutoka nchi 16 watashiriki, ambapo majaji watano watasimamia mashindano ya Qur'ani Tukufu na majaji wengine watano wa mashindano ya Sunnah, wote ni wataalam wa kusoma Qur'ani na sayansi ya Hadithi.
Mashindano hayo yanalenga kukuza misimamo ya Kiislamu ya wastani miongoni mwa vijana, kwa kuzingatia mafundisho ya Qur'ani na Sunnah, kwa mujibu wa waandaaji.
Tukio hili litajumuisha duru ya kufuzu ya siku tatu, na kilele chake ni sherehe ya kufunga Oktoba 19.
3490274