IQNA

Mashindano ya Qur'ani na Sunna

Mashindano ya Kwanza ya Kimataifa y Qur'an na Sunna Afrika Magharibi nchini Mauritania

10:36 - October 17, 2024
Habari ID: 3479603
IQNA - Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani na Sunnah kwa nchi za Afrika Magharibi yalianza Jumanne na  nchini Mauritania.

Sherehe za ufunguzi zilifanyika Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania, kwa kushirikisha maafisa wa Mauritania na Saudia.

Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania Sidi Yahya Ould Sheikhna alisisitiza katika hotuba yake kwamba Qur'an na Sunna za Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ni misingi ya Uislamu wa kweli.

Ameashiria kuwa, tukio hilo la Qur'ani Tukufu na Sunnah ni matokeo ya ushirikiano kati ya Mauritania na Saudi Arabia hususan katika nyanja ya sayansi ya Qur'ani na mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW).

Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yanalenga kuimarisha mafungamano ya vijana na Quran na Sunnah, kuwahimiza kunufaika na mafundisho yenye mwanga na mwongozo wa maandiko hayo matukufu.

Abdulaziz bin Abdullah Al-Raqabi, Balozi wa Saudia huko Nouakchott, pia alizungumza katika hafla hiyo, akibainisha kuwa juhudi zilifanywa ili kuhakikisha mashindano hayo yanakidhi viwango vya juu vya uadilifu na uwazi.

Ameongeza kuwa, "Kuichagua Mauritania kuwa mwenyeji wa tukio hili kubwa la kimataifa ni ushahidi wa uhusiano wa kina na wa kindugu kati ya watu wa Saudi Arabia na Mauritania."

Mashindano haya yameandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Mauritania, kwa usaidizi na usimamizi wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia.

Tukio hilo lina washiriki 136 kutoka nchi 16 ambao watashindana katika makundi makuu mawili: kuhifadhi Qur'ani na kuhifadhi Hadithi za Mtume.

Majaji watano watawatathmini washindani katika kitengo cha Qur'ani, huku jopo jingine la wataalamu watano waliobobea katika Hadithi likiwatathmini washiriki katika sehemu ya Sunnah.

Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yamegawanyika katika makundi manne: kuhifadhi kikamilifu Quran kwa mitindo saba ya kisomo, pamoja na Tajweed na tafsiri ya Juzuu 10 za mwisho za Qur'ani; uhifadhi kamili wa Qur'ani kwa Tajweed na tafsiri ya Juzuu 10 za mwisho; kuhifadhi Juzuu 20 Qur'ani kwa Tajweed; na kuhifadhi Juzuu 10 za Quran kwa Tajweed.

Katika sehemu ya Sunnah, washiriki wanashindana katika kuhifadhi maneno ya Mtume Muhammad (SAW) kutoka katika vitabu na vyanzo vilivyochaguliwa.

Mashindano hayo yalioyoanza Oktoba 15 yanamalizika leo Oktoba 17, huku sherehe za kufunga na utoaji wa tuzo zikipangwa JumamosiOktoba 19.

 4242716

Habari zinazohusiana
captcha