IQNA

Mtizame Qarii Badr Hussein akisoma Sura An-Nisaa

17:46 - June 16, 2020
Habari ID: 3472869
TEHRAN (IQNA) – Sheikh Mohammad Badr Hussein alikuwa qarii mashuhuri wa Misri katika zama zake.

Sheikh Badr Hussein alizwaliwa katika familia ya wasomaji na wanaohifadhi Qur'ani mwaka 1937 nchini Misri katika jimbo la Gharibia.

Alianza kujifunza kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri mdogo na alijiunga na Radio ya Qur'ani nchini Misri mwaka 1961 na mwaka 1963 akatauliwa kuwa qarii rasmi katika televisheni ya Misri.

Mwaka 1970 Sheikh Badr Hussein alishiriki katika mashindano ya Qur'ani nchini Malaysia na akafanikiwa kupata nafasi ya kwanza. Halikadhalika aliwahi kuwa jaji katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kimataifa.

Hii hapa chini ni klipu ya Marhum Sheikh Badr Husseni akisoma sehemu ya Sura an-Nisa katika Qur'ani Tukufu.  

3905004

Kishikizo: misri qarii Badr Hussein
captcha