IQNA

Swala ya Ijumaa katika miji 157 ya Iran baada ya kusitishwa miezi miwili kutokana na COVID-19

18:11 - May 08, 2020
Habari ID: 3472745
TEHRAN (IQNA) - Swala ya Ijumaa imeswaliwa kusaliwa hii leo katika miji mikubwa na midogo ipatayo 157 na mikoa 21 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baada ya kusitishwa tokea mapema mwezi Machi mwaka huu kutokana na mripuko wa ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Hotuba za Ijumaa zimefupishwa hii leo, na ibada hiyo imefanyika kwa kufuata na kuchunga taratibu zote za kiafya.

Ali Nouri, Afisa Mratibu wa Baraza la Upangaji Sera za Maimamu wa Sala ya Ijumaa amesema Sala na amesema Swala ya Ijumaa imeswaliwaa katika 'maeneo meupe', ambayo hayana tena hatari ya ugonjwa wa COVID-19. Aidha Swala ya Ijumaa haikuswaliwa katika makao makuu ya mikoa na maeneo ambayo yanaendelea kuripoti kiwango kikubwa cha kesi za maambukizi ya corona.

Sala za Ijumaa na shughuli nyingine za mijumuiko zilikuwa zimesitishwa hapa nchini tokea mapema mwezi Machi, kutokana na mlipuko wa corona.

Hata hivyo hivi karibuni, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu alisema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa Iran imefanikiwa pakubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 ikilinganishwa na nchi nyingine za dunia; na kwamba hadi hivi sasa karibu miji 157 imetangazwa kuwa ni sehemu nyeupe nchini Iran hivyo maeneo matukufu na ya ibada katika sehemu hizo yamefunguliwa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Iran, maeneo meupe ni yale ambayo maambukizi ya corona yatakuwa ni sifuri kwa muda wa wiki moja na hakuna mtu aliyefariki dunia kwa corona katika kipindi hicho, na idadi ya waliopata afueni ikawa imeongezeka na hali hiyo ikaendelea pia katika wiki ya pili.

Hadi hivi sasa waathiriwa zaidi ya 82 elfu wa ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata nafuu na afya njema na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.

2710906

captcha