IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Mashujaa wa Yemen lazima watatoa somo kali kwa mabeberu hao wa dunia

19:08 - January 12, 2024
Habari ID: 3478188
IQNA-Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran amesema kuwa, leo hii Yemen shujaa inaungwa mkono kila upande na kwamba licha ya kupita siku 100 tangu utawala wa Kizayuni uanzishe jinai zake kila upande lakini imeshindwa kufikia malengo yake huko Ghaza.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad Hossein Abu Turabi Fard amesema hayo na kuongeza kuwa, Msemaji wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa naye amekiri kwamba muqawama wa Gaza haushindiki kwani ni aiodolojia madhubuti na hii ina maana ya kukiri rasmi kushindwa Marekani, utawala wa Kizayuni na madola ya Magharibi kwenye vita vya Ghaza.

Hayo yamekuja baada ya komandi ya jeshi la anga la Marekani kusema kuwa jeshi hilo limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya zaidi ya shabaha 60 na vituo 16 vya kijeshi vya Yemen kwa kutumia makombora 100 ya kuongozwa kwa mbali. 

Kwa upande wake jeshi la Yemen limesema kuwa, Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi 73 leo alfajiri dhidi ya mikoa tofauti ya Yemen na kuahidi kutoa majibu makali kwa mabeberu hao.

Baada ya tamko hilo la jeshi la Yemen, Baraza la Kisiasa la Serikali ya San'a nalo limetoa taarifa na kusema kuwa, popole yalipo maslahi ya Marekani na Uingereza ni shabaha halali ya Yemen katika majibu yake makali yatakayokuja dhidi ya madola hayo ya kiistikbari. 

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Mohammad Hossein Abu Turabi Fard akilaani mashambulizi hayo ya leo ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen na kusema kuwa, mashujaa wa Yemen lazima watatoa somo kali kwa mabeberu hao wa dunia. 

4193060

Habari zinazohusiana
captcha