IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Mauaji ya wanawake na watoto, Gaza ni chanzo cha chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani

20:57 - February 28, 2025
Habari ID: 3480280
IQNA-Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa, adui wa Israel sio kambi ya Muqawama tu na kuongeza kuwa, mauaji ya wanawake na watoto huko Gaza na makamanda wa Muqawama yamesababisha kusambaa duniani kote chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani.

Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Kadhim SIddiqui amesema hayo leo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Swala ya Ijumaa hapa mjini Tehran na kubainisha kwamba, hii leo chuki dhidi ya Marekani na Israel inashuhudiwa kila mahali duniani ambapo kunasikika nara na kaulimbiu ya kifo kwa Marekani na kifo kwa Israel.

Akiashiria mazishi na maziko ya Mwanajihadi Mkubwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Shahidi Sayyid Hashim Safiyyuddin, Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran amezungumzia sira na mwenendo wa jihadi wa Sayyid Nasrullah na kueleza kuwa, mwanamapambano huyo alikuwa mwiba mkali kwa maadui katika kipindi cha uhai wake.

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake za Swala ya Ijumaa Sheikh Kadhim Seddiqi ameashiria kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani na kueleza kwamba, toba ndio vazi la kuelekea katika mwaliko wa Ramadhani.

Aidha amesema, Ramadhani ni mwezi mtukufu ambao kwa hakika ni fursa ya kipekee na maalumu kwa Umma wa Mtume Mtukufu (SAW) ambapo vitabu vya mbinguni pia vilishushwa katika mwezi wa Ramadhani.

4268737

 

 

Habari zinazohusiana
captcha