IQNA

12:46 - May 18, 2020
News ID: 3472778
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Bujuma Albaz, Imamu na Khatibu katika Msikiti wa Mohammad wa Sita katika mji wa Bouznika ana sauti nzuri na yenye mvuto ya kusoma Qur'ani yenye kushabihiana na ile ya qarii mashuhuri wa Misri Abdul Basit Abdul Swamad.

Kwa mujibu wa tovuti ya al3omk Bujuma Al-Baz ana sati ya kipekee ya usomaji Qurani kiasi kwamba katika msikiti anakoswalisha, mamia ya waumini hufika hapo kusikiliza qiraa yake.

Katika mahojiano na gazeti la Al Amq anasema yeye hutajwa na wengi kama 'Abdul Basit wa Morocco. Kuhusu alivyoweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu anasema: "Baba yangu alinihimiza kuhifadhi Qur'ani. Miaka ya nyuma kila familia ilikuwa inachagua mmoja kati yao awe hafidh wa Qur'ani na hapo mimi nilichaguliwa."

3899714

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: