IQNA

15:42 - June 02, 2020
News ID: 3472826
TEHRAN (IQNA)- Naibu Spika wa Bunge la Iraq Hassan Karim al-Kaabi ametoa wito kwa Saudi Arabia kukarabati Makaburi ya Baqii katika mji mtakatifu wa Madina.

Katika taarifa Jumatatu, al-Kaabi ametoa wito kwa Saudia kukarabati makaburi hayo yenye Maimamu watoharifu wa kizazi cha Mtume Muhammad SAW.

Aidha ametoa wito kwa mashirika ya kimatiafa na nchi za Kiislamu kuishinikiza Saudia kukarabati turathi hiyo muhimu ya Kiislamu.

Itakumbukwa kuwa siku kama ya leo miaka 92 yaani tarehe 8 Shawwal mwaka 1345 (1925) Mawahabi walibomoa makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume SAW ambayo yako Baqii, katika mji mtakatifu wa Madina.
Baada ya Muhammad Ibn Saud kutawala tena baadhi ya maeneo ya Hijaz, ukiwemo mji wa Madina, Sheikh Abdullah bin Bulaihad aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kiwahabi, alitoa fatuwa ya kubomolewa makaburi matukufu na ya kihistoria ya mjini Madina.
Mawahabi walikusanya watu kwa nguvu na kuwalazimisha kwenda katika makaburi hayo ya Baqii na kuanza kubomoa na kuharibu kila kitu kilichokuwa juu ya makaburi ya mji huo na nje ya mji. Miongoni mwa makaburi yaliyobomolewa na kuharibiwa vibaya ni makaburi manne ya .maimamu na wajukuu wa Mtume SAW

Hadi leo watawala wa Saudi Arabia wanaendelea kuharibu turathi za kale za Kiislamu nchini humo kwa visingizio mbali mbali.

Mawahabi wanaotekeleza uharibifu huo wanakusudia kufuta kabisa kumbukumbu zote za historia adhimu ya Uislamu ambapo hivi sasa miji mitakatifu ya Makka na Madina inaendelea kushuhudia maeneo mengi ya historia ya Kiislamu yakimbomolewa.../mh

Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Shawwal mwaka 1345 (1925) Mawahabi walibomoa makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume SAW ambayo yako Baqii, katika mji mtakatifu wa Madina.
Baada ya Muhammad Ibn Saud kutawala tena baadhi ya maeneo ya Hijaz, ukiwemo mji wa Madina, Sheikh Abdullah bin Bulaihad aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kiwahabi, alitoa fatuwa ya kubomolewa makaburi matukufu na ya kihistoria ya mjini Madina.
Mawahabi walikusanya watu kwa nguvu na kuwalazimisha kwenda katika makaburi hayo ya Baqii na kuanza kubomoa na kuharibu kila kitu kilichokuwa juu ya makaburi ya mji huo na nje ya mji. Miongoni mwa makaburi yaliyobomolewa na kuharibiwa vibaya ni makaburi manne ya .maimamu na wajukuu wa Mtume SAW

Hadi leo watawala wa Saudi Arabia wanaendelea kuharibu turathi za kale za Kiislamu nchini humo kwa visingizio mbali mbali.

Mawahabi wanaotekeleza uharibifu huo wanakusudia kufuta kabisa kumbukumbu zote za historia adhimu ya Uislamu ambapo hivi sasa miji mitakatifu ya Makka na Madina inaendelea kushuhudia maeneo mengi ya historia ya Kiislamu yakimbomolewa.

3902526

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: