Misikiti nchini humo ilifungwa miezi kadhaa iliyopita kufuatia kuibuka janga la corona. Mwezi agosti swala za jamaa zilianza tena katika misikiti ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa, waumini wote watatakiwa kuvaa barakoa kabla ya kuingia msikitini na pia viwango vya joto mwilini vitapimwa mlangoni.
Halikadhalika Waislamu walio ndani ya msikiti watatakiwa kutokaribiana na misikiti itakuwa ikisafishwa mara kwa mara kwa kutumia dawa za kuua virusi.
Uzbekistan ni nchi ya Asia ya Kati. Imepakana na Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Turkmenistan.
Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Miji yake kama vile Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 Kabla ya Miladia (BC). Nchi hiyo ni mashuhuri kwa misikiti yake na asilimia 96 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu. Asilimia 80 ya wakaazi wa nchi hiyo ni Waislamu.