IQNA

‘Halal TV’ kuzinduliwa Korea Kusini

13:08 - September 09, 2020
Habari ID: 3473152
TEHRAN (IQNA) – Korea Kusini imetangaza mpango wa kuzinduliwa televisheni itakayojulikana kama ‘Halal TV’ kwa lengo la kuwavutia watalii Waislamu nchini humo.

Shirika la Utalii la Korea Kusini limetangaza kuwa Televisheni hiyo ambayo awali itaruhisa matangazo yake kupitia mtandao wa YouTube inalenga kutoa taarifha kuhusu huduma halali hasa migahawa yenye kupika chakula halali katika mji mkuu wa nchi hiyo, Seoul.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirika la Utalii la Kore Kusini, watalii wengi Waislamu nchini humo hukerwa na ukosefu wa migahawa yenye chakula halali. Kwa msingi huo kumekuwa na mkakati maalumu wa kuanzisha migahawa halali nchini humo.

Korea Kusini inawavutia watalii Waislamu nchini humo ili watembelee maeneo yenye mvuto na pia na pia wapate matibabu katika kile kinachojulikana kama utalii wa kitiba.

Mwaka huu wa 2020 Korea Kusini imepata pigo kubwa katika sekta ya utalii kutokana na janga la corona ambapo utalii umepungua kwa asilimia 74.

3472515/

Kishikizo: korea kusini ، halal ، watalii ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :