IQNA

Binti Muislamu Marekani apigwa marufuku mechi ya voliboli kutokana na kuvaa Hijabu

12:30 - September 19, 2020
Habari ID: 3473183
TEHRAN (IQNA) – Binti Muislamu mwanafunzi wa shule ya upili amepigwa marufuku kucheza mechi ya voliboli baada ya refa kudai kuwa vazi lake la Hijabu linakiuka sheria.

Najah Aqeel ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tisa latika chuoe cha Valor Collegiate Acaemies, uko Nashville, Tennessee, alikuwa acheze mechi ya voliboli Jumanne. Lakini kabla ya mechi refa alimfahamisha Najah na kocha wake kuwa vazi lake la Hijabu linakiuka sheria za Shirikishe la Kitaifa la Michezi ya Shule za Upili (NFHS) ambalo lina jukumu la kuainisha sheria za michezo ya shule za upili kote Marekani.  Alifahamishwa kuwa anahitaji idhini maalumu kucheza jambo ambalo Najah na kocha wake walisema hawakuwa wanalifahamu. Najah anasema amewahi kucheza mechi kadhaa akiwa amevaa Hijabu na alikasirishwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu swalo hilo. Mama haye Najah, Aliya Aqeel, ambaye alifika kumtazama binti yake alicheza alishtushwa na taarifa hiyi. Najah naye alilia n kusikitishwa na tukio hilo.

Wanafunzi wa kike Marekani wamekuwa wakipigwa marufuku kushiriki katika michezo kutokana na kuvaa Hijabu. Hata nje ya shule pia wanariadha Waislamu wanakumbana na matatizo ya kubaguliwa kutokana na vazi lao la Hijabu.

3472597

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :