IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu Marekani

Polisi New York matatani kwa kumvua mwanamke Hijabu kinyama

21:58 - January 19, 2024
Habari ID: 3478218
IQNA - Mwanamke Mwislamu ambaye alikamatwa na Idara ya Polisi ya Kaunti ya Suffolk (SCPD) huko New York mnamo 2022 anaishtaki idara hiyo kwa kukiuka haki zake na kumsababishia madhara ya kisaikolojia baada ya maafisa kuvua hijabu yake kwa nguvu.

Mwanamke huyo, Marowa Fahmy, anasema maafisa wa polisi walimvua kwa nguvu hijabu yake na kumgusa isivyofaa wakati wa msako wa mwili mbele ya maafisa wa kiume. Anasema pia kwamba polisi hawakumrudishia hijabu yake kwa saa kadhaa baada ya kuachiliwa, licha ya maombi yake ya mara kwa mara.

Kesi hiyo, iliyowasilishwa Jumatano na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) tawi la New York na inatafuatilia fidia kwa Fahmy na kupinga sera ya SCPD ya kumvua hijabu, ambayo inaiita " isio na ubinadamu, ina inayo kaidi waziwazi sheria."

Mawakili wanasema kitendo hicho cha kumvua mwanamke Hijabu ni kinyume cha sheria za Jimbo la New York na shirikisho zinazolinda uhuru wa kidini na kupiga marufuku ubaguzi unaotegemea dini.

"CAIR-NY inasisitiza kwamba haki za Waislamu Wamarekani haziishii kwenye milango ya kituo cha polisi," alisema Burhan Carroll, mwanasheria wa CAIR-NY. "Tutaendelea kuwatetea wanajamii wetu ambao wamedhulumiwa na vyombo vya sheria. Tunatumai kuwa uwasilishaji huu utaleta haki kwa Bi Fahmy na utawalinda wengine dhidi ya madhara ya siku zijazo."

3486863

Habari zinazohusiana
Kishikizo: marekani cair hijabu
captcha