IQNA

Waislamu Marekani

Kituo cha Kiislamu huko Milwaukee chaandaa hafla ya kuadhimisha Hijabu

20:44 - February 11, 2024
Habari ID: 3478337
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Dawah cha Milwaukee nchini Marekani kimeandaa hafla ya Henna & Hijab siku ya Jumamosi, Februari 3, kuheshimu Hijabu inayovaliwa na wanawake wa Kiislamu.

Tukio hilo lilikuwa na aina mbalimbali za hijabu, abaya, na mavazi mengine ya kawaida ya kuuza, pamoja na wasanii wa hina ambao walipamba mikono ya washiriki, Jarida la Wisconsin Muslim liliripoti Ijumaa.

Waandalizi hao Fardowsa Mohamed na Mako Shidad walisema wanataka kusherehekea vazi la Hijabu ikiwa ni ishara ya ibada, kujithamini na kujipenda hasa katika kipindi hiki ambacho hijabu zinakabiliwa na ubaguzi na ukatili.

Walisema wameshangazwa na watu waliojitokeza. Tukio hilo lilichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa, kuanzia saa nane alasiri hadi saa moja usiku, kutokana na shauku ya waliohudhuria.

Mojawapo ya matukio muhimu katika tukio hilo ilikuwa ni mafunzo ya hijab ya Dada Hadja, mhamiaji kutoka Guinea, ambaye alionyesha njia tofauti za kuvaa na kufunga hijabu.

Kituo cha Milwaukee Islamic Dawah kitaandaa hafla nyingine yenye mada ya hijab, Cover Girls: Journey and Struggle with Self-love, Jumamosi, Feb. 17, saa nane alasiri.

 

 

 

3487140

 

 

 

 

Kishikizo: hijabu marekani waislamu
captcha