IQNA

18:07 - September 22, 2020
Habari ID: 3473193
TEHRAN (IQNA)- Benki ya Jaiz Plc ya Nigeria imetajwa kuwa benki ya Kiislamu iliyoimarika zaidi duniani mwaka 2020.

Tuzo ya Kimataifa ya Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu (GIFA) imetoa  zawadi hiyo kwa Benki ya Jaiz na kusema benki hiyo imechaguliwa kutokana na kuimarisha shughuli zake za kutoa huduma kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Mbali na kutambuliwa kutokana na kuzingatia sheria za Kiislamu katika huduma zake, benki hiyo pia imetambuliwa kutokana na jitihada za kuimarisha maisha ya wafanyakazi wake na jamii kwa ujumla. Mkurugenzi wa GIFA, Profesa Humayoun Dar amemuandikia barua Mkurugenzi Mkuuwa Benki ya Jaiz Hassan Usman na kupongeza kwa mafanikio hayo.

Kwa upande wake, Usman ametoa shukrani zake zake kwa GIFA kutokana na zawadi hiyo ambayo ni ishara ya wazi kuwa juhudi za benki hiyo zinatambuliwa kimataifa.

3924590

Kishikizo: nigeria ، benki ya kiislamu ، jaiz
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: