IQNA

Watunisia wataka ‘siku ya kupambana na Uzayuni’ itambuliwe katika kalenda

20:23 - October 02, 2020
Habari ID: 3473224
TEHRAN (IQNA) – Wanaharakati wa kisiasa nchini Tunisia wametaka Oktoba Mosi itambuliwe nchini humo kama ‘Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uzayuni.’

Wanaharaakti hao wameyasema hayo katika maandamano ya Alhamisi kwa mnasaba wa mwaka wa 31 tokea utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleza hujuma ya kigaidi ya kulipua bomu katika makao makuu ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO).

Haya yanajiri siku chache baada ya Rais wa Tunisia, Kais Saied kutoa mwito kwa walimwengu kushirikiana kuhakikisha kuwa Wapalestina wanakombolewa kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni na wanapata haki zao.

Septemba 15, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na utawala wa kiimla wa Bahrain zilisaini makubaliaono ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ikulu ya White House nchini Marekani, na kusaliti malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

Njama za tawala za kidikteta za Kiarabu za kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni zinafanyika katika hali ambayo, kwa miaka mingi Wazayuni wanawakandamiza Wapalestina na wanafanya jinai za kila anuai katika maeneo mbalimbali ya Kiarabu na Kiislamu.

3926722

Kishikizo: tunisia palestina israel
captcha