IQNA

Maandamano yaendelea Bahrain kupinga uhusiano na Israel

21:33 - October 03, 2020
Habari ID: 3473228
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Bahrain wameandamana tena Ijumaa katika mji mkuu Manama na miji mingine kupunga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Pamoja na kuwepo ukandamizaji mkubwa na kamata kamata ya wanaharakati, mamia walijitokeza katika maandamano yaliyopewa jina la ‘Ijumaa ya Kuangamia Mapatano ya Kihaini.”

Walioshiriki maandamano walisikika wakitoa nara kama vile ‘Mauti kwa Marekani’, ‘Mauti kwa Israel’ na ‘Ijumaa ya Kuangamia Mapatano ya Kihaini.”

Waandamanaji kadhaa walikamatwa.

Maandamano hayo yalifanyika wakati Yossi Cohen, mkuu wa shirika la kijasusi la utawala haramu wa Israel,  Mossad, alipokuwa safarini Bahrain kwa lengo la kufanya mazungumzo na wakuu wa nchi hiyo.

Tarehe 15 mwezi wa Septemba mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Bahrain walisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu katika ikulu ya rais wa Marekani, White House mjini Washington.  Hadi hivi sasa ulimwengu mzima wa Kiislamu bali hata baadhi ya nchi zisizo za Waislamu, kama Afrika Kusini zinalaani kitendo hicho cha kisaliti cha Bahrain na UAE. Hatua hiyo ya UAE na Bahrain imetajwa kuwa ni usaliti kwa kwa malengo ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.

 

3472701

captcha