IQNA

21:54 - November 15, 2020
News ID: 3473361
TEHRAN (IQNA) - Imedokezwa kuwa, Rais mteule wa Marekani, Joe Biden anatazamiwa kuangalia upya uhusiano wa karibu uliopo hivi sasa baina ya nchi hiyo na Saudi Arabia.

Wataalamu na wadadisi wa mambo wamenukuliwa na mashirika ya habari ya Marekani wakisema kuwa, baada ya Biden kukabidhiwa hatamu za uongozi, Riyadh na Washington hazitakuwa tena na uhusiano wa kirafiki kama ilivyoshuhudiwa katika kipindi cha uongozi wa Donald Trump.

Shirika la NBC News la Marekani limefichua kuwa, Saudia haitastafidi tena na uhusiano mzuri na wa kidugu na Marekani kama ilivyoshuhudiwa katika kipindi cha Biden.

Biden amepania kuhitimisha vita vya muungano vamizi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen, ambavyo vimeua watu zaidi ya 112,000 tokea mwaka 2015. Kadhalika amedokeza kuwa utawala wake utasimamisha mauzo ya silaha kwa watawala wa Saudia.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Democratic amekuwa akiukosoa utawala wa kidikteta wa Riyadh kwa mienendo yake ya kukanyaga haki za binadamu, na hususan baada ya mauaji ya Jamal Khashoggi, aliyekuwa mwandishi wa habari na mkosoaji mkubwa wa wa ukoo wa Aal-Saud.

Trump alimkingia kifua wazi wazi Muhammad Bin Salman, Mrithi wa Ufalme wa Saudia, ambaye anatuhumiwa kutoa amri ya kutekelezwa mauaji hayo ya kikatili ya Oktoba mwaka 2018 katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki.

Hayo yanajiri wakati ambao, kuendelea kwa mzozo wa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani uliozushwa na Rais Donalld Trump ambaye alikuwa mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi huo, kupanuka mzozo huo na kutolewa madai mapya kumetajwa kuwa ni tahadhari kubwa kuhusiana na matokeo mabaya kwa Marakeni.

Trump amekataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais na anawachochea waungaji mkono wake kufanya maandamano mitaani wakipinga matokeo ya zoezi hilo na kufungua mashtaka mahakamani kwa madai ya kufanyika udanganyifu.  

3473113

Tags: saudi arabia ، biden ، Trump ، marekani
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: