IQNA

Mwanazuoni maarufu wa Qur’ani Jordan aaga dunia

22:01 - November 21, 2020
Habari ID: 3473380
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni mashuhuri wa Qur’ani Tukufu nchini Jordan, Mustafa al-Mashni ameaga dunia baada ya kuugua corona au COVID-19.

Al Mashni alikuwa mtaalamu wa sayansi za Qur’ani na Tafsiri. Aidha alifunza Qur’ani Tukufu katika Chuo Kikuu cha Yarmouk nchini Jordan na pia katika taasisi kadhaa za ulimwengu wa Kiarabu.

Jumuiya ya Wanazuoni Jordan imetuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia mwanazioni huo.

Wanazuoni na wasomi kadhaa wa Kiislamu duniani wamepoteza maisha kutokana na corona.

Virusi vya corona vimesababisha vifo vya watu 1,373,381 tangu kuzuka kwake mwezi Desemba huko China. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa takwimu kutoka kwenye vyanzo rasmi zilizokusanywa na Shirika la Habari, AFP. Visa vilivyoripotiwa vimefikia 57,583,290 ambapo miongoni mwa hivyo watu 36,725,500 wanatazamwa kamba ndio waliopona. Kulingana na takwimu za jana, duniani kote kuliripotiwa vifo vipya 11,847 na maambukizi 657,054. Kwa mujibu wa majumuisho hayo, mataifa yaliyobainika kuwa na vifo vingi vipya ni pamoja na Marekani yenye vifo 1,878, Ufaransa vifo 1,138 na Mexico 719. Marekani ambayo imeathirika vibaya na janga hilo, ina jumla ya vifo 254,424 kutoka katika maambukizi 11,913,945. Takriban watu 4,457,930 wameripotiwa kupona virusi vya corona.

3936327

 

Kishikizo: jordan ، qurani tukufu ، mashni
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha