IQNA

10:52 - December 14, 2020
Habari ID: 3473455
TEHRAN (IQNA) – Baraza la Kiislamu Singapore (Muis) limetoa wito kwa Waislamu nchini humo kukubali chanjo ya COVID-19 wakati itakapopatikana na itakapopati idhini ya idara husika za afya kuwa ni salama kutumia.

Muongozo wa baraza hilo umesema Waislamu wanaruhusiwa kutumia chanjo ya COVID-19 kwani ni hitajio muhimu la kulinda maisha wakati huu w janga la COVID-19.

Taarifa hiyo imesema kwa ujumla mchakato wa utegenezaji wa chanjo ulizingatia mafundisho ya Kiislamu na kuongeza kwamba Uislamu unalipa umuhimu mkubwa suala la maisha hivyo ni muhimu kutumia chanjo hiyo.

Waziri wa Masuala ya Kidini Singapore Masagos Zulkifli amekaribisha muongozo wa Muis na amewahimiza Waislamu wachanjwe punde chanjo hiyo itakapopatikana Singapore.

3473394

Kishikizo: waislamu ، singapore ، covid-19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: