Haya yalitangazwa na Naibu Waziri wa Masuala ya Kiislamu, Faishal Ibrahim, siku ya Jumamosi alipokuwa akizungumza kuhusu mpango huo.
Nyamba ya Udhiya kawaida huchinjwa wakati wa sikukuu ya Idul Adha.
Ameeleza kuwa mchango huo ni kielelezo cha dhamira ya umma wa Kiislamu wa Singapore katika kuunga mkono juhudi za kibinadamu kimataifa. “Hatua hii haioneshi tu utekelezaji wa wajibu wetu wa kidini, bali pia ni ishara ya mshikamano wetu na ndugu zetu wanaokabiliwa na matatizo,” alisema. “Inaonesha namna ibada zetu zinavyoweza kuwafikia walio katika dhiki.”
Usambazaji wa nyama hiyo utafanywa na washirika wa kimataifa, wakiwemo Shirika la Msaada wa Kifalme wa Jordan (Jordan Hashemite Charity Organisation).
Udhiya ni ibada tukufu katika Uislamu inayohusisha kuchinja wanyama kama vile kondoo au mbuzi, ambapo nyama hugawiwa kwa waumini na watu wasiojiweza. Nchini Singapore, shughuli hii huratibiwa kitaifa kupitia SalamSG, jukwaa linaloshughulikia shughuli za misikiti nchini humo.
Mchango huu wa nyama ya Udhiya unaoelekezwa Gaza unafuatia kampeni kubwa ya "Msaada kwa Gaza 2025", ambayo ilikusanya zaidi ya dola milioni 2.4 za Singapore kati ya mwezi Februari na Aprili. Fedha hizo zitatumika kusaidia mahitaji ya msingi kama huduma za afya na elimu kwa familia zilizoathirika.
3493631