IQNA

21:09 - December 19, 2020
Habari ID: 3473472
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Algeria imetoa wito wa kufunguliwa tena madrassah za Qur’ani nchini humo kwa kuzingatia kanuni za kiafya katika kipindi hiki cha janga la COVID-19 au corona.

Katika taarifa, jumuiya hiyo imesema kama ambavyo shule za msingi na upili zimefunguliwa, madrassah za Qur’ani nazo zinaweza pia kufunguliwa.

Wanazuoni hao wamesisitiza kuwa madrassah za Qur’ani zianze kuwapokea wanafunzi kwa kuzingatia kanuni zote za afya za kuzuia maambukizi ya corona.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, madrassah za Qur’ani zina nafasi muhimu katika malezi ya wanafunzi bora nchini Algeria.

Halikadhalika wanazuoni hao wametoa wito kwa Waalgeria wote kushirikiana katika vita dhidi ya corona.

Hadi kufikia Disemba 19, waliambukizwa corona Algeria walikuwa wamefika 94,371 huku waliofariki wakiwa ni 2,647.

3941757

Kishikizo: algeria ، qurani tukufu ، covid 19
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: