IQNA

Harakati za Qur'ani

Wizara ya Wakfu Algeria kusambaza nakala za Qur'ani kwa Lugha ya Ishara

20:47 - January 08, 2025
Habari ID: 3480018
IQNA – Waziri wa Wakfu Algeria amesema kuwa Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara itatolewa kwa wale wenye ulemavu wa kusikia nchini humo.

"Tunafanya kazi kuwasilisha Qur'ani kwa lugha ya ishara kwa ndugu zetu viziwi, na Surah za mwanzo za Qur'ani tayari zimeandaliwa kwa lugha ya ishara," alisema Youcef Belmehdi, An-Nahar iliripoti.

Aliyasema hayo kando ya semina ya kitaifa juu ya kuimarisha utambulisho wa kitaifa na kidini wa Algeria.

Alisisitiza hatua zilizochukuliwa na wizara kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum na kwa kukuza mafundisho ya kidini katika jamii na kusema kuwa uchapishaji wa "Arbaeen Nawawi" (mkusanyiko wa hadithi zinazochukuliwa kuwa zenye itibari kubwa na Waislamu wa madhehebu ya Sunni) umeanza, na vitabu "Fiqh Mukhtasar na Imam Khudari Al-Jazairi" na "Al-Mukhtasar fi Al-Ibadat" viko katika mchakato wa kuchapishwa.

Belmehdi pia alibainisha kuwa idadi ya wanafunzi wa Qur'ani katika shule za Qur'ani na Zawayas (vituo vya jadi vya Qur'ani) nchini Algeria imefikia milioni 1.2, na idadi hiyo inaongezeka wakati wa likizo za kiangazi.

3491375

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu algeria
captcha