IQNA

Wanazuoni 16 wa Kishia wamekamatwa Saudi Arabia

18:46 - December 22, 2020
Habari ID: 3473482
TEHRAN (IQNA) - Wanazuoni zaidi ya 12 wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia wanashikiliwa bila kufunguliwa mashtaka nchini Saudi Arabia huku ufalme huo ukishadidisha ukandamizaji wa jamii za waliowachache nchini humo.

Kwa mujibu wa Radio Al Nour ya Lebanon, wakuu wa Saudia hivi karibuni walimkamata Sheikh Hussein al-Nimr, mwanae Sheikh Nimr Baqr al-Nimr, mwanazuoni wa Kishia kutoka mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo ambaye  alinyongwa kidulma mwaka 2016.

Wakaazi wengi wa mkoa wa mashariki mwa Saudia wenye utajiri mkubwa wa mafuta ni  Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Ripoti ya Radio Al Nour imesema wakuu wa Saudia wamekiri kumkamata Sheikh Hussein Al Nimr siku mbili baada ya kuenea ripoti kuwa ametekwa nyara. Hivi sasa jumla ya wanazuoni 16 wa Kishia wamekamatwa katika maeneo ya Qatif na al Ahsa mashariki mwa Saudia  na wanashikiliwa gerezani kinyume cha sheria.

Radio al Nour imewataja wanazuoni wengine wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia waliokamatwa Saudia kuwa n pamoja na Sayyed Hashim al-Shaks, Hussein al-Radhi, Mohammad al-Habib, Sayyed Ja'far al-Alawi, Mohammad al-Ebad, Abdullatif al-Nasser, Badr Al Talib, Mohammad Zainuddin, Habib al-Khabbaz, Hassan Al Zayed, Samir al-Hilal, Abdul-Jalil Al-Athiyan , Abbas al-Mazani, Sayyed Khidr al-Awami na Abbas al-Saeed.

Utawala wa Saudia umeshadidisha kamatakamata ya wapinzani wakiwemo wasomi wa Kiisalmu, waandishi na watetezi wa haki za binadamu hasa katika Mkoa wa Mashariki.

Mkoa huo umekuwa medani ya maandamano ya amani kila Ijumaa tokea Februari mwaka 2011. Waandamanaji wanataka mabadiliko, uhuru wa kujieleza, kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa na kuhitimishwa ubaguzi wa kiuchumi na kidini dhidi ya eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa mafuta.

Maandamano hayo yamekumbana na ukandamizaji mkali wa vikosi vya utawala wa Kifalme wa Saudia.

3473475

captcha