IQNA

20:21 - December 25, 2020
Habari ID: 3473490
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imekosoa uungaji mkono wa baadhi ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa hujuma hizo ni tishio kwa usalama na uthabiti katika eneo.

Katika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema utawala wa Kizayuni wa Israel haungethubutu kutekeleza hujuma zake kama si uungaji mkono usio na mipaka wa Marekani na nchi zingine kadhaa.

Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema kuwa, mapema Ijumaa ya leo, kwa mara nyingine ardhi ya Syria imelengwa kwa makombora ambayo yalivurumishwa kutoka anga ya Lebanon. Taarifa hiyo imesema hujuma hiyo ni ukiukwaji wa wazi wa azimio nambari 250 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Makombora hayo yalitua katika eneo la Masyaf kati mwa Syria.

Duru za habari zinadokeza kuwa ndege za kivita za utawala haramu wa Israel mapema Ijumaa zilikiuka anga ya Lebanon na kuvurumisha makombora hayo yaliyolenga Syria.

3943256

Kishikizo: syria ، israel
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: