IQNA

10:04 - January 18, 2021
News ID: 3473569
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq maarufu kama Al-Hashdu-Sha'abi au PMU amesisitiza ulazima wa kutekelezwa agizo la bunge la nchi hiyo la kutaka askari wa jeshi la Marekani waondoke nchini humo.

Mkuu wa PMU asisitiza kuondoka askari vamizi wa Marekani nchini IraqFalih al-Fayyaz ametoa sisitizo hilo Jumapili alipohutubia mkoani Al Anbar kusini mwa Iraq wakati wa khitma ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na  naibu kamanda wa PMU Abu Mahdi al-Muhandis.  Al Fayyaz ameeleza kwamba, Wairaqi wamethibitisha kuwa, wao ni waaminifu kwa makamanda wao wanamapambano, hawakubali kuburuzwa na kulazmishwa, na nchi yao haitafuata na kutii utawala wa nchi nyingine.

Al Fayyaz aidha amelaani hatua ya wizara ya fedha ya serikali inayotawaliwa na migogoro ya rais Donald Trump wa Marekani ya kumwekea yeye vikwazo pamoja na mkuu wa vikosi vyote vya Al-Hashdu-Sha'abi Abu Fadak al Muhammadawi na akabainisha kwamba, Marekani haiko kwenye nafasi ya kuipa uwezo wa kutoa maagizo na amri kuhusiana na makamanada wa taifa la Iraq.

Askari wajeshi vamizi la Marekani wamepiga kambi nchini Iraq tangu mwaka 2003; na kambi yao kubwa kabisa ya kijeshi ya Ainul-Asad iko kwenye mkoa wa Al Anbar magharibi mwa nchi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq.

Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Watu wengine wanane waliokuwa katika msafara huo nao pia waliuawa shahidi.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Pia alikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa eneo vipande vipande.

Baada ya mauaji hayo ya kigaidi ya makamanda hao wawili, Bunge la Iraq liliitisha kikao na kutaka jeshi la kigaidi la Marekani liondoke nchini Iraq.

Wananchi wengi na makundi mbalimbali ya Wairaqi wanataka askari wa jeshi la kigaidi la Marekaniwaondoke nchini mwao.

3948292

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: