IQNA

Hania ampongeza Kiongozi Muadhamu kwa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

15:36 - February 11, 2021
Habari ID: 3473641
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa mkono wa pongezi na kheri kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Ismail Hania Jumatano  alimtumia ujumbe Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kuwa, harakati ya Hamas na wananchi wa Palestina wako pamoja na wananchi wa Iran katika kusherehekea sherehe hizo kubwa; na akatoa shukrani na pongezi zake kubwa kwa Iran kwa misimamo yake madhubuti katika kuunga mkono malengo, taifa na mapambano makubwa ya Wapalestina kwa ajili ya kutetea haki zao za kisheria. 

Wananchi wa Iran jana Jumatano tarehe 22 mwezi Bahman kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani walisherehekea maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu; na licha ya  hatua zote za udhibiti kutokana na maambukizi ya corona, wananchi katika mji wa Tehran na mikoa mingene ya Iran walimiminika mitaani ili kudhihirisha kufungamana kwao na misingi na thamani za Mapinduzi ya Kiislamu.

Washiriki katika hamasa hiyo kubwa ya maandamano hayo aidha wametangaza kuendeleza muqawama wa pande zote na kuendelea kufanya kazi na kutoa huduma bora ili kutatua matatizo na kusisitiza kuwa, kumuogopa adui ni kosa kubwa na lisilosameheka.

3953447

captcha