IQNA

10:18 - March 27, 2021
News ID: 3473764
TEHRAN (IQNA)- Zoezi la kuwasajili washiriki wa Awamu ya 14 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Televisheni ya Al Kauthar linaendelea.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yatafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu wa 1442 Hijria Qamaria.

Mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Kiislamu ya Al Kauthar TV Bw. Abbas Razavi amesema usajili ulianza katika siku ya tatu ya mwezi huu wa Shaaban kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Imam Hussein AS.  Aidha amesema siku ya mwisho ya kujisajili ni Aprili 8 2021. Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ambayo huandaliwa na Televisheni ya Al Kauthar yamepewa aya ya Qur’ani Tukufu isemayo  إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu".  (Qur’ani Tukufu 78:31).

Mashindano hayo, ambayo yametajwa kuwa kati ya makubwa zaidi ya aina yake duniani, hufanyika kwa njia ya simu au intaneti.

Anayetaka kushiriki anapaswa kujaza fomu maalumu na kutuma faili ya sauti ya qiraa yake ya Qur'ani Tukufu isiyozidi dakika mbili. Jopo la majaji katika mashindano hayo ni wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi kadhaa za Kiislamu duniani.

Kwa maelezo zaidi na kujisajili katika mashindano hayo, bonyeza hapa.

3961090

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: