IQNA

Misri kuruhusu Sala katika baadhi ya Misikiti Mwezi wa Ramadhani

22:39 - March 31, 2021
Habari ID: 3473775
TEHRAN (IQNA)- Misri imesema itaruhusu Sala ya Tarawih katika baadhi ya misikiti tu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakuu wa misri wamesema misikiti hiyo itatakiwa kuzingatia kanuni zote za afya za kuzuia maambukizi ya COVID-19 na sala hiyo haitazidi nusu saa.

Aidha serikali ya Misri imetangaza kupiga marufuki mijumuiko yote misikiti na futari za mitaani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Misri imesema itapokea dozi 854,000 za chanjo ya COVID-19  katika fremu ya ule mpango wa kimataifa wa COVAX. Aidha nchi hiyo hivi karibuni ilipokea dozi laki sita za chanjo ya COVID-19 kutoka shirika la Sinopharm la china. Hadi sasa watu 11,914 wamepoteza maisha kutokana na corona nchini Misri kati ya 200,739 walioambukizwa.

3474330

Kishikizo: misri Corona ramadhani
captcha