Kwa mujibu wa tovuti ya royanews.tv Kamati Kuu ya Kupambana na COVID-19 nchini Oman Jumatatu imetangaza kuwa, Sala ya Tarawih ni marukufu katika misikiti yote nchini humo.
Halikadhalika kamati hiyo imetangaza sheria ya kutotoka nje kuanzia kuanzia saa tatu usiku hadi saa 10 alfajiri kuanzia Aprili 8.
Kamati Kuu ya Kupambana na COVID-19 nchini Oman pia imetangaza marufuku ya mijumuiko yote ya futari au shughuli zingine misikitini na maeneo mengine katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.