IQNA

Misri, UAE zapiga marufuku Mijumuiko ya Futari mwezi wa Ramadhani

20:08 - March 08, 2021
Habari ID: 3473716
TEHRAN (IQNA) – Wakuu wa Misri na baadhi ya maeneo ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na wametangaza kuwa mijumuiko ya umma ya Futari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni marufuku ili kuzuia kuenea virusi vya Corona au COVID-19.

Aidha mbali na kupiga marufuku mijumuiko ya Futari katika umma nchi hizo mbili pia zimepiga marufuku Itikafu misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baraza la Misaada na Wakfu katika eneo la Ajman nchini UAE limetangaza kubatilisha vibali vyote vya mijumuiko ya futari katika ummah wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Baraza hilo limesema mashirika yote ya misaada UAE yanapaswa kupiga marufuku mijimuiko ya Futari na pia kuhakikisha chakula kinachosambazwa kwa wasiojiweza kina viwango vya juu.

Nchini Misri pia serikali imetangaza kuwa Sala ya Tarawih na Itikafu misikitini ni marufuku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuzuia kuenea COVID-19.

3958309

Kishikizo: misri futari uae ramadhani
captcha