IQNA

Biden amteua jaji wa kwanza Muislamu Marekani katika ngazi ya fiderali

23:16 - April 06, 2021
Habari ID: 3473789
TEHRAN (IQNA)- Rais Joe Biden wa Marekani amemteua Mpakistani-Mmarekani, Zahid Qureishi kuwa jaji wa mahakama katika ngazi ya fiderali nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani kwa Mwislamu Mmarekani kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Quraishi ambaye ni mwenyeji wa New Jersey  alikuwa hakimu kwa muda wa miaka mitatu na akiidhinishwa, atakuwa Muislamu wa kwanza kuhudumu kama jaji wa fiderali au katika ngazi ya jimbo nchini Marekani.

Biden amempendekeza Qureishi kuwa jaji wa kifiderali katika Mahakama ya New Jersey. Gavana wa jimbo hilo, Phil Murphy, Seneta Corey Booker na Seneta Bob Menendez wamempongeza Rais wa Biden kwa uamuzi huo.

Aidha Kamati ya Masuala ya Umma ya Marekani-Pakistan nayo pia imempongeza Biden kwa kumpendekeza Quraishi kushika wadhifa huo.

Jaji Qureishi alihudumu katika Jeshi la Marekani kama mwendesha mashtaka na alitumwa vitani Iraq mwaak 2004-2006. Aidha alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya markeani kama mwendesha mashtaka wa kifiderali katika huko New Jersey.

Kwa mujibu wa sheria ya Marekani, baada ya jaji wa fiderali au jimbo kuteuliwa na rais, bunge la Seneti lina jukumu la kumuidhinisha.

3961867

captcha