IQNA

13:03 - April 29, 2021
Habari ID: 3473859

Mashindano ya Qur'ani Peshawar, Pakistan

TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Pakistan kimeandaa mashindano ya Qur'ani katika mji wa Peshawar kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashindano ya Qur'ani Peshawar, Pakistan

Mashindano hayo ya siku mbili yamemalizika leo Aprili 10 na yalijumuisha kuhifadhi Qur'ani Tukufu, na pia ufahamu wa Sura Israa na Sura Hujurat.

Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa kuwafanya vijana waifahamu Qur'ani na mafundisho yake sambamba na kuisoma katika mwezi wa Ramadhani.

Kituo cha utamaduni cha Iran mjini  Peshawar hujihusisha na harakati mbali mbali za kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kuandmaa mashindano ya Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani.

3967752

captcha