IQNA

Iran kuwapokea na kuwatibu Wapalestina waliojeruhiwa katika hujuma za utawala wa Kizayuni Ghaza

20:16 - May 17, 2021
Habari ID: 3473919
TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa iko tayari kuwapokea na kuwapa matibabu bila malipo Wapalestina ambao wamejeruhiwa katika hujuma za kinyama za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa, mkuu wa Shirika la Matibabu ya Dharura Iran amesema shirika hilo liko tayari kutuma timu za huduma za dharura za kitiba kwa ajili ya kuwasaidia waliojeruhiwa katika hujuma ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Ghaza. Aidha amesema Shirika la Matibabu ya Dharura Iran liko tayari kuwaleta Wapalestina waliojeruhiwa nchini Iran ili wapata matibabu ya kitaalamu zaidi.

Hadi sasa Wapalestina karibu 218, wakiwemo watoto 58, wameuawa shahidi katika  hujuma hii mpya ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Ghaza huku wengine zaidi ya 1,235 wamejurhiwa.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi dhidi ya Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hii kuandamana kulalamikia vikali ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem). Kitendo cha askari katili wa Israel kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kimehesabiwa kuwa ni kuvuka mstari mwekundu wa Wapalestina na Waislamu duniani.

Katika kujibu jinai hizo za Israel makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamevurumisha mamia ya makombora katika miji ya Israel ukiwemo mji wa Tel Aviv na kusababisha hasara kubwa.

84332071

Kishikizo: ghaza palestina israel iran
captcha