IQNA

Spika wa Bunge la Iran

Mdundo wa moyo wa umma wa Kiislamu kwa ajili ya Palestina

14:09 - May 16, 2021
Habari ID: 3473915
TEHRAN (IQNA)- Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu nchini Iran (Bunge) amesema kuwa moyo wa Umma wa Kiislamu unaendelea kudunda kwa ajili ya Palestina, na Umma na makundi ya mapambano dhidi ya Uzayuni yataendelea kusimama kidete na kutetea malengo ya ukombozi wa Palestina.

Muhammad Baqir Qalibaf ameyasema hayo mapema leo katika ufunguzi wa kikao cha wazi cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu mjini Tehran. Amelaani mashambulizi ya kikatili yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kigaidi wa Israel dhidi ya watu wa Palestina na kusema kuwa, utawala huo unawalenga raia wa kawaida katika mashambulizi makubwa na ya kinyama.

Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa, moyo wa Umma wa Kiislamu unaendelea kudunda kwa ajili ya Palestina na Umma na makundi ya mapambano yamesimama kidete kulinda malengo na thamani za ukombozi wa Palestina na hapana shaka maghasibu wa Kizayuni watapata jazaa na malipo yao. 

Qalibaf pia ametangaza uungaji mkono na himaya yake kwa wanamapambano wa Kipalestina na kuendelea kusimama kwao imara dhidi ya wanajeshi makatili wa Israel. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikipaza sauti kubwa kupinga ukatili wa Wazayuni dhidi ya watu wa Palestina hususan raia wa Ukanda wa Gaza na imeitaka jamii ya kimataifa kutelekeza wajibu wake wa kuwalinda raia hao.

Itakumbuwka kuwa, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amefuta safari yake rasmi nchini Austria akipinga hatua ya nchi hiyo ya kupeperusha bendera za utawala haramu wa Israel juu ya majengo ya serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Vienna, huku Israel ikiendelea kuwaua kinyama raia wa Palestina.

Tokea Jumatati hadi sasa Wapalestina 170, wakiwemo watoto 41, wameuawa shahidi katika  hujuma hii mpya ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Ghaza huku wengine 1,000 wakijeruhiwa.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi dhidi ya Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hilo kuandamana kulalamikia vikali ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem). Kitendo cha askari katili wa Israel kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kimehesabiwa kuwa ni kuvuka mstari mwekundu wa Wapalestina na Waislamu duniani.

Katika kujibu jinai hizo za Israel makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamevurumisha mamia ya makombora katika miji ya Israel ukiwemo mji mkuu Tel Aviv na kusababisha hasara kubwa. Waisraeli  wasiopungua 7 wameangamizwa katika oparesheni hizo za ulipizaji kisassi za Wapalestina. 

3971709

captcha