IQNA

"Nyoyo zetu ziko pamoja nanyi", Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu awaambia Wapalestina

19:55 - May 24, 2021
Habari ID: 3473941
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Ali Khamenei amejibu barua za viongozi wa harakati za mapambano ya kukomboa Palestina za Hamas na Jihad Islami akisisitiza kuwa: Nyoyo zetu ziko pamoja nanyi katika uwanja wa mapambano yenu, na hatimaye mtapata ushindi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jumatatu ya leo  Ayatullah Ali Khamenei amejibu barua za Ismail Hania Mkuu wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina na ile ya Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina Ziad Al-Nakhaleh akisema, mapambano na maghasibu wanaoikalia Palestina kwa mabavu ni mapambano dhidi ya dhulma, ukafiri na ubeberu na kuongeza kuwa: Nyoyo zetu ziko pamoja nanyi katika medani za mapambano na dua zetu zinazowaombea ushindi wa kudumu zinaendelea siku zote. 

Katika jibu lake kwa barua ya Ismail Hania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas, Ayatullah Khamenei amesema mapambano yenu ni mapambano dhidi ya dhulma, ukafiri na ubeberu na kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu mtashinda mapambano hayo na ardhi takatifu itasafishwa na kutwahirishwa kutokana na uchafu wa maghasibu. 

Sehemu moja ya barua ya Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Katibu Mkuu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina imesema: Jihadi kubwa na ushindi wenu ndugu zangu wa Palestina imewafurahisha wapenzi  wenu kote duniani; nyoyo zetu zipo katika uwanja wa mapambano yenu, na dua zetu zinazowaombea muendelee kupata ushindi zinaendelea siku zote. 

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita na baada ya Israel kulazimika kusitisha vita dhidi ya wakaza wa Ukanda wa Gaza viongozi wa Hamas na Jihad Islami walimtumia barua mbili tofauti kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wakimpongeza kwa ushindi huo. 

Sehemo moja ya barua ya Katibu Mkuu wa Jihad Islami ilisema: "Himaya ya misaada yako ya kudumu katika nyanja zote imekuwa na nafasi na mchango mkubwa zaidi katika mapigano ya "Panga la Quds" na mafanikio yake. Wanamapambano wa Kipalestina, wamesimama kidete na kwa ushujaa mkubwa katika medani ya vita licha ya nguvu kubwa ya kijeshi ya adui." 

Ziad Al-Nakhaleh alisisitiza kuwa: "Naona lazima kumkumbuka shahidi kipenzi na kamanda mpendwa wetu Haj Qassem Soleimani ambaye amepata daraja ya juu ya kuuliwa shahidi. Tunamkumbuka na kumhisi zaidi Kamanda Soleimani katika nyakati hizi za kihistoria."    

3973458

captcha