IQNA

12:33 - June 12, 2021
Habari ID: 3473998
TEHRAN (IQNA)- Kijana Mpalestina ameuawa shahidi Ijumaa baada ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamejitokeza katika maandamano ya amani kupinga ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni.

Aidha Wapalestina kadhaa wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika katika miji ya Nablus, Qalqilya na Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Wanajeshi katili wa Israel waliwatwanya waandamanaji kwa kutumia risasi, hai, risasi za plastiki na gesi ya kutoa machozi.

Wizara ya Afya ya Palestina imethibitisha kuuawa shahidi kijana huyo na kuongeza kuwa Wapalestina wengine sita wamejeruhiwa. 

Aliyeshuhudia tukio hilo amesema Mohammad Said Hamayil aliyekuwa na umri wa miaka 15 aliuawa shahidi baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel.

Kwa mujibu wa takwimu, kuna walowezi wa Kizayuni wapatao 650,000 wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds (Jerusalem) Mashariki.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Ukingo wa Magharibi na Quds ni maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na hivyo ujenzi wa vitongoji ni kinyume cha sheria.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha maazimio kadhaa za kuutaka utawala wa Kizayuni uondoke katika ardhi za Palestina ambazo unazikaliwa kwa mabavu.

3976795

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: