IQNA

9:15 - July 03, 2021
Habari ID: 3474065
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewahujumu Wapalestina waliokuwa wakiandamana kwa amani dhidi ya ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika mji wa Nablus ulio katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Duru zinaarifu kuwa baada ya Sala ya Ijumaa, wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel waliwashambulia Wapalestina waliokuwa wakiandamana dhidi ya kitongoji cha Eviatar katika eneo la Jabal Sabih mjini Beita.

Shirika rasmi la habari la Palestina , WAFA, limeandika kuwa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel walitumia risasi za plastiki kuwatawanya waandamanaji ambapo, Wapalestina 150 waliokuwa wakiandamana kwa amani wamejeruhiwa na saba miongoni mwao wamelazwa hospitalini.

Kitongoji haramu cha Eviatar kimekuwa kitovu cha mvuntano baina ya Wazayuni na Wapalestina.  Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanautaka utawala wa Israel utekeleza amri ya mahakama ambayo imetaka walowezi wa Kizayuni waondolewe katika kitongoji hicho.

Kwa mujibu wa azimio nambari 2334 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, shughuli zote za Israel za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni kinyume cha sheria. Hata hivyo utawala wa Kizayuni unakaidi marufuku hiyo, kila leo unavunja nyumba za Wapalestina, kuwapora ardhi na mashamba yao na kujenga vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni bila ya kuchukuliwa hatua yoyote na Umoja wa Mataifa.

3475120

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: