IQNA

Uchaguzi nchini Iran

Kiongozi Muadhamu apiga kura, asema siku ya uchaguzi ni siku ya taifa

11:01 - June 18, 2021
Habari ID: 3474017
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei alikuwa wa kwanza kutumbukiza kura yake kwenye sanduku la kupigia kura mapema leo katika kituo cha Husainiya ya Imam Khomeini (MA) mjini Tehran.

Baada ya kupiga kura Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, siku ya uchaguzi ni siku ya taifa na kuongeza kuwa: Leo wananchi ndio wenye uwanja na medani na kwa kura zao wanaainisha ramani ya nchi kwa ajili ya miaka kadhaa ijayo, hivyo leo ni siiku yao.

"Akili na mantiki vinahukumu kwamba wananchi wote wanapaswa kushiriki katika mtihani huu mkubwa wa kitaifa na kwamba zoezi hili la kuchagua rais linawafaidisha wananchi wenyewe na kuipaisha juu Jamhuri ya Kiislamu katika medani za kimataifa. Kura ya kila raia ina umuhimu mkubwa." Aidha amesisitiza kuwa, wote wanapaswa kupiga kura na mtu hapaswi kusema kura yake moja haitakuwa na faida kwani ni hiyo kura moja ambayo ikijumuishwa na kura zingine huwa ni mamilioni ya kura za wananchi.

Zaidi ya Wairani milioni 59 elfu 310, (milioni 29, 980,000,38 wanaume na milioni 29,330,000, 269 wanawake) wamekamilisha masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa leo wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia ucahguzi wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji.

3978228

captcha