IQNA

Ujumbe wa Rais Rouhani baada ya wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi

18:55 - June 19, 2021
Habari ID: 3474020
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi kumepelekea taifa la Iran lipate ushindi katika kukabiliana na maadui.

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo katika ujumbe alioutuma Jumamosi ambapo amewashukuru wananchi wa kujitokeza kwa wingi kaika uchaguzi. Amesema kujitokeza wananchi katika zoezi la upigaji kura jana ni ishara kuwa wanafungamana na malengo matakatifu ya Imam Khomeini MA na pia  wameitikia wito wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Rouhani amesema vita vya kisaikolojia vya maadui si tu kuwa havikuzuia wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura bali pia ni sababu ya kupoteza matumaini maadui na wasiolitakia mema taifa la Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshukuru wananchi wa Iran kwa kuwa na subira wakati wa vita vya kiuchumi na mashinikizo ya kidhalmu ya adui. Rais Rouhani amesema rais mteule atakuwa na jukumu nzito la kutumia uwezo wote wa nchi ili kuweza kutekeleza matakwa ya wananchi. 

Zaidi ya Wairani milioni 59 waliokuwa wametimiza masharti ya kupiga  jana walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa rais ambao ulikuwa wa wagombea wanne baada ya Wagombea wengine watatu kujiondoa katika mchuano huo Jumatano.

Bada ya kumalizika zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran imetangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo ulioshirikisha mamilioni ya wapiga kura.

Kwa mujibu wa taarifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abdolreza Rahmani Fazli ametangaza matokeo hayo leo Jumamosi mbele ya waandishi wa habari hapa jijini Tehran na kusema kuwa, wapiga kura milioni 28 na laki tisa na 36 elfu na nne wameshiriki katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesema, asilimia 48.8  ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura wameshiriki kwenye uchaguzi huo. Ameongeza kuwa, Sayyid Ebrahem Raeisi ndiye aliyechaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kura milioni 17 na laki 9 na 25,345 za wananchi.

3978521

Kishikizo: iran ، rouhani ، uchaguzi ، raeisi
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :