IQNA

Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu apongeza ungaji mkono wa Iran kwa Palestina

0:26 - March 28, 2022
Habari ID: 3475083
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa taifa la Palestina.

Ziyad al-Nakhalah aliashiria kushindwa kwa baadhi ya tawala za Kiarabu kudhoofisha harakati za mapambano ya Kiislamu kwa kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni, Al-Ahed News iliripoti.

Amesema wametambua kuwa watu wa Palestina ambao wamezingirwa wanaweza kupinga uvamizi huo na kupambana na adui.

Ameongeza kuwa, miongoni mwa nchi za Kiislamu, Iran pekee ndiyo inayolipa gharama ya kuiunga mkono Palestina.

Katika ulimwengu huu ambao umejaa dhuluma, Iran imesimama upande wa watu wa Palestina na inaendelea kuwaunga mkono, alisema.

Kwingineko katika matamshi yake, Nakhalah amesisitiza ulazima wa kuwepo umoja zaidi kati ya makundi ya Wapalestina na kuimarishwa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni.

4045120

captcha