IQNA

Kadhia ya Palestina

Iran: Mataifa ya Kiislamu yatetee kivitendo haki za Wapalestina

17:01 - August 05, 2024
Habari ID: 3479233
IQNA-Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, ametoa wito kwa serikali za Kiislamu kuunga mkono haki za Wapalestina kwa ufanisi zaidi.

Kan'ani amesema hayo Jumapili jijini Tehran kwa mnasaba wa mnasaba wa "Siku ya Haki za Binadamu za Kiislamu na Utukufu wa Kibinadamu," na kueleza kwamba, Uislamu ndio mnadi mkuu wa haki za kimaada na kimaanawi za mwanadamu.

Kan'ani ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X: Kama ambavyo katika zama za ujahilia, Uislamu ulizungumza juu ya haki ya kuishi na utu wa mwanadamu na kutoa adabu za maisha ya heshima, leo hii serikali na mataifa ya Kiislamu yanastahiki kuwa wadai wakubwa na wabeba viwango wa kweli wa haki za binadamu na waendelezaji wa mafundisho na maadili haya ya Kiislamu yenye thamani kubwa.

Wakati huo huo, duru ya nane ya utoaji Tuzo za Haki za Binadamu za Kiislamu ilifanyika jana hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran Sheikh Gholam Hossein Mohseni Ejeie, maafisa wa ngazi za juu na mabalozi wa nchi za Kiislamu wanaoishi mjini Tehran.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran sambamba na kubainisha misimamo ya Tehran kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel amesisitiza udharura wa kuweko mshikamano wa ulimwengu mkabala wa utawala huo ghasibu.

3489389

Kishikizo: palestina shahidi Haniya
captcha