IQNA

Muqawama

Hafla nchini Yemen kuwaenzi wanafunzi wa Qur'ani na kumuenzi Shahidi Haniya

16:55 - August 05, 2024
Habari ID: 3479232
IQNA - Sherehe ilifanyika katika mji wa Ta'iz, Yemen, kuadhimisha kuhitimu kwa wanafunzi 721 wa Qur'ani.

Walikuwa wamechukua kozi ya Qur'ani iliyofanywa na vituo kadhaa vya kuhifadhi Qur'ani mjini humo. Tukio hilo pia lilimkumbuka Shahidi Ismail Haniya, ambaye aliuawa mjini Tehran wiki iliyopita. Mwandaaji huyo aliamua kuandaa hafla  hizo za kuwaenzi washiriki wa kozi ya Qur'ani baada na pia kumuenzi shahidi Haniya katika shambulio la kigaidi la Israel jijini Tehran. Idadi kubwa ya watu na maafisa wa kidini, Qur'ani na kisiasa walishiriki katika hafla hiyo huko Ta'iz. 
Nasr Abdul Ghani Mutahhar, afisa wa kamati ya maandalizi alihutubia katika hafla hiyo na kuwataka wahitimu kujaribu kuwa mfano wa kuigwa katika masuala ya maadili ya Qur'ani, ukweli na uchamungu. Vile vile alimsifu Shahidi Haniya na watu wa Ukanda wa Gaza ambao wamekuwa wakijitolea mhanga maisha yao kwa ajili ya Umma wa Kiislamu.

3489384

Habari zinazohusiana
Kishikizo: shahidi Haniya
captcha