IQNA

21:49 - August 22, 2021
Habari ID: 3474216
TEHRAN (IQNA) - Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) imetangaza kuanza kukubali maombi ya toleo la 5 la mashindano ya Qur'ani kwa wanawake.

Ibrahim Bu Milha, mshauri wa Mtawala wa Dubai katika Masuala ya Utamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya DIHQA, alisema mashindano hayo ambayo yanajulikana kama Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum, ni miongoni mwa programu kuu za DIHQA.

Alisema awamu hii ya tano ya mashindano ilikuwa imecheleweshwa kwa sababu ya janga la corona.

Kufuatia kufanikiwa kwa mashindano ya wanaume katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kamati iliamua kufanya mashindano hayo kwa wanawake pia..

Kulingana na afisa huyo, wanawake ambao wametambulishwa rasmi na nchi yao au wana makazi ya UAE na wanaweza kuwakilisha nchi yao wataweza kushiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Alisema washiriki wanapaswa kuwa na umri wa miaka 25 au chini na waweze kuhifadhi Qur'ani nzima na kuzingatia sheria za Tajweed.

Mwisho wa usajili Septemba 15, Bu Melha, alisema, akiongeza kuwa wale walio tayari kuhudhuria mashindano wanaweza kujiandikisha kupitia barua pepe ya info@quran.gov.ae

3992196

Kishikizo: dihqa ، mashindano ya qurani ، dubai
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: