IQNA

Wanajesthi wa utawala wa Kizayuni wavamia Msikiti wa Al Aqsa

20:48 - September 11, 2021
Habari ID: 3474281
TEHRAN (IQNA)- Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel ijumaa walivamia Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) wakati Wapalestina walipokuwa wakiandamana kubainisha kufungamana na wenzao wanaoteswa katika jela za Israel.

Makundi ya Palestina yalikuwa yameitisha  maandamano kuwaunda mkono wafungwa Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel huku maandamano mengine yakiwa ni yale ya kila wiki ya kupinda ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Wakuu wa magereza ya kuogofya ya Israel wameweka sheria kali na kandamizi zaidi baada ya wafungwa sita kutoroka kwa kuchimba njia ya chini ya ardhi wiki iliyopita. Tayari wafungwa sita waliotoroka wameshatekwa nyara tena na askari wa Israel.

Alfajiri Jumatatu iliyopita mateka hao sita walichimba njia ya chini ya ardhi na kufanikiwa kutoroka jela ya Gilboa yenye ulinzi mkali ya utawala haramu wa Israel. Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa usalama wa utawala wa Kizayuni katika pande kadhaa.

Kwanza ni kuwa, utawala wa Israel kabla ya tukio hilo ulijaribu pakubwa kuyazuia makundi ya mapambano huko Lebanon na Palestina kuchimba mahandaki na njia za kupitia chini ya ardhi; hata hivyo sasa mateka wa Kipalestina wamefanikiwa kutoka jela ya Israel yenye ullinzi mkali baada ya kuchimba njia ya chini ya ardhi yenye urefu wa makumi ya mita.

 Kuhusu kutoroka mateka sita wa Kipalestina katika jela ya Gibloa ya utawala wa Kizayuni gazeti la al Quds al Arabi limeripoti kwamba: "Inaonekana kuwa oparesheni hiyo ni kubwa na pana zaidi ya kutoroka mateka hao sita wa Kipalestina; kwa sababu harakati hiyo si pigo kwa walinda jela na uongozi wa jela ya Gilboa peke yao bali ni pigo kwa hadhi na taswira ya serikali mpya ya Naftali Bennet, Waziri Mkuu wa utawala huo; serikali ambayo inakosolewa kwa utendaji dhaifu. 

3475675

Kishikizo: aqsa palestina wafungwa
captcha