IQNA

13:54 - September 17, 2021
News ID: 3474305
TEHRAN (IQNA) - Makumi ya walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel, na kuuvunjia heshima msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.

Walowezi hao  wa Kizayuni baada ya kuingia katika eneo la ndani la msikiti huo mtakatifu, wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa utawala bandia wa Israel, walisikika wakipiga nara dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Kufuatia uvamizi huo dhidi ya msikiti wa al-Aqsqa kuliibuka mapigano baina yao na wananchi Waislamu wa Palestina. Muhammad Hammadah, mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina amesema kuwa, harakati hiyo imetoa agizo kwa Wapalestina kuwa tayari na katika tahadhari kwa ajili ya kuutetea msikiti wao huo mtakatifu

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kwa kuyazayunisha maeneo hayo na kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.

3998057

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: