IQNA

22:25 - September 16, 2021
News ID: 3474302
TEHRAN (IQNA)- Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amedai kuwa jeshi la nchi yake limemuangamiza Adnan Abou Walid al-Sahrawi, kinara wa tawi kundi la kigaidi la ISIS au Daesh Magharibi mwa Afrika (ISWAP).

Rais wa Ufaransa ametangaza kifo cha kiongozi huyo usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi kwenye ukurasa wake ya Twitter.

"Haya ni mafanikio mapya makubwa katika mapigano tunayoendesha dhidi ya makundi ya kigaidi huko Sahel," Macron ameandika ujumbe wa Twitter.

 Aliuawa pamoja na wenzake kadhaa ambao walikuwa wakijaribu kuondoka kaskazini mwa Mali kwenda nchi jirani ya Niger.

Adnan Abou Walid al-Sahrawi, mwenyeji wa Sahara Magharibi, awali alikuwa kinara wa zamani wa kundi la magaidi wakufurishaji wa Mujao (Movement for Uniqueness and Jihad in West Africa) na kisha kinara wa tawi kundi la kigaidi la ISIS au Daesh Magharibi mwa Afrika (ISWAP).tangu kuundwa kwake mnamo 2015.

Wakati huo, Abou Walid al-Sahrawi alitangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh; na kundi lake lilikuwa likihesabiwa kuwa moja ya matawi ya kigaidi ya Daesh athirifu zaidi  barani Afrika; ambalo mwaka 2019 na 2020 lilifanya mashambulizi mengi. 

Abou Walid al-Sahrawi alikuwa adui wa umma katika eneo linalojulikana kama mipaka mitatu - Mali, Burkina Faso na Niger - ambapo kundi lake bado linaendesha ukatili mkubwa.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni walisisitiza kuwa, Afrika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2021 imedhurika na kujipenyeza pakubwa makundi ya kigaidi ya Daesh na al Qaida.

Wamesema, kujipenyeza pakubwa makundi ya kigaidi ya Daesh na al Qaida katika baadhi ya nchi za Kiafrika kama Mali, Burkina Faso, Kodivaa, Niger, Senegal, Nigeria, Cameroon, Somalia, Kenya, Msumbiji na Tanzania ni jambo lenye kutia wasiwasi. 

Makundi ya magaidi wakufurishaji barani Afrika kama vile ISWAP, Boko Haram na Al Shabab, ambao wamewasababishia watu wa bara hilo hasara kubwa, hufuata itikadi kali ya Uwahhabi ambayo ni itikadi rasmi nchini Saudi Arabia.

3997984

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: