IQNA

21:41 - December 04, 2021
Habari ID: 3474639
TEHRAN (IQNA)- Magaidi wa kundi la ISIS au Daesh wameua askari saba wa Jeshi la Nigeria kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa magaidi wa ISWA, tawi la ISIS Magharibi mwa Afrika, wakiwa wanaendesha magari kadhaa ya pick up walishambulia kituo cha wanajeshi wa Nigeria katika mji wa Rann ulio kilomita 175 kutoka Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno.

Jeshi la Nigeria halijatoa taarifa kuhusu hujuma hiyo.

Kundi la ISWAP ilijitenga na kundi  la kigaidi la Boko Haram na limekuwa likitekeleza hujuma za mara kwa mara dhidi ya askari wa Nigeria.

Jimbo la Borno ni kitovu cha magaidi wakufurishaji wanaofuata pote la Uwahhabi na wamekuwa wakishambulia pia nchi jirani za Chad, Cameroon na Niger. Kwa mujibu wa taarifa za Umoja wa Mataifa tokea hujuma za kigaidi zianze eneo hilo mwaka 2009 hadi sasa watu takribani 300,000 wameuawa na mamilioni wengine  wanategemea misaada sasa baada ya shughuli zao za kimaisha kuvurugwa na magaidi.

Mwezi Oktoba jeshi la Nigeria lilidai kumuua kinara wa ISWAP katika oparesheni ya kijeshi.

4018213

Kishikizo: nigeria ، borno ، ISWAP ، isis au daesh ، boko haram
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: