IQNA

Kiongozi Muadhamu katika mkutano na wanamichezo wa Olimpiki na Paralimpiki

Utawala haramu wa Israel unatafuta uhalali kupitia michezo ya kimataifa

20:52 - September 18, 2021
Habari ID: 3474308
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema, kutotambuliwa na kususiwa utawala ghasibu wa Israel katika michezo ni jambo muhimu sana.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo Tehran wakati alipokutana na wanamichezo waliotwaa medali katika mashindano ya Paralympic na Olimpiki ya Tokyo Japan na kueleza kwamba, utawala unaomwaga damu, unaouawa watoto na haramu wa Israel unafanya juhudi za kujipatia uhalali kupitia medani za kimataifa za michezo.

Ameongeza kuwa mabeberu wa dunia nao wamekuwa wakiusaidiia utawala huo dhalimu, hata hivyo maafisa wa michezo na wanamichezo hawapaswi kuwa na kiguguymizi cha aina yoyote katika katika uwanja huu.

Kiongozi Muadhamu amesema mwanamichezo wa Iran hawezi kamwe kupeana mkono na mwakilishi na utawala utendao jinai wa Israel kwani kufanya hivyo ni sawa na kuutmabua utawala huo.

Amesema kadhia sawa nah ii imewahi kutekndak miaka ya nyuma kwani wanariadha wan chi nyingi walikataa kushindana na wawakilishi wa utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini na baada ya muda mfupi utawala huo ulisambaratika na hivyo utawala wa Kizayuni nao pia utaangamizwa.

Kwingineko katika hotuba yake, Ayatullah Khamenei  amewapongeza wanamichezo hao kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika mashindano hayo ya Olimpiki na Paralimipiki yaliyomalizika hivi karibuni.

Amesema kuwa, ujumbe muhimu zaidi wa ushindi wa wanamichezo wanaoliletea fakhari taifa lao katika mashindano ya kimataifa ni kufanya mambo ambayo kidhahiri yanaonekana haiwezekani kuyafanya, na kufikisha ujumbe wa kusimama kidete, matumaini na nishati kwa jamii na vijana.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria na kutoa mifano ya mabingwa na watwaa medali katika michezo ya dunia kwa njia isiyo salama na sahihi na kubainisha kwamba, dhulma ya marefa, rushwa na mambo ya kisiasa, kutumia dawa za kuongeza nguvu  ambazo zimepigwa marufuku, kuchukua medali kwa kuuza nchi na mwanamichezo kujiuza ni mifano ya wazi ya ubingwa usio salama.

Ayatullah Khamenei amesema kuwa, dhihirisho la thamni za kiutu, kidini na kimaanawi sambamba na ubingwa michezoni ni jambo lenye thamani mno.

Kiongozi Muadhamu ameashiria mashindano ya michezo ya Olimpiki na Paralympic na kusema kuwa, wanawake wanamichezo wa Kiirani wamethibitisha katika michezo hiyo kwamba, vazi la hijabu siyo kizuizi cha kung'ara michezoni kama ambavyo wamethibitisha hilo katika medani nyingine kama za kisiasa, kielimu na uongozi.

3998127

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha