IQNA

Jinai za Israel

Mashinikizo ya kutaka Israel ipigwe marufuku katika michezo ya Olimpiki ya Paris

16:56 - July 25, 2024
Habari ID: 3479182
IQNA-Wito unaongezeka kote ulimwenguni wa kuipiga marufuku timu ya utawala haramu wa Israel kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 inayoanza Ijumaa huku utawala huo ukiendeleza vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya raia Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Wanaharakati wanaoiunga mkono Palestina wamezindua lebo ya #BanIsraelFromParisOlympics kwenye mitandao ya kijamii ili kuweka shinikizo kwa waandalizi kuzuia ushiriki wa wanariadha wa Israel katika Michezo iliyopangwa kuanza tarehe 26 Julai.

Wakati huo huo 

Shirika moja la haki za binadamu lenye makao yake nchini Marekani linasema utawala katili wa Israel unapaswa kuzuiwa kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 kutokana na uamuzi wa hivi majuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu jinai za kinyama za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Fadi Quran, mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Avaaz, alitoa kauli hiyo katika chapisho la mtandao wa kijamii siku ya Jumanne kufuatia maoni ya ushauri ya ICJ ambayo ilisisitiza kuwa Israel inatekeleza ubaguzi wa rangi na wa kimfumo dhidi ya Wapalestina na imechukua sehemu kubwa ya eneo lao kupitia uvamizi wake.

Quran alisema "Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ina sera inayokataza ubaguzi na ubaguzi wa kimfumo, na hivyo ni lazima kupigwa marufuku" wale wanaojihusisha na vitendo kama hivyo," na kuongeza, "ICJ imethibitisha kuwa Israel ina hatia ya vitendo hivi."

Akisisitiza kuwa kuwepo kwa wawakilishi wa Israel katika hafla ya kimataifa ya michezo kunakiuka kanuni za Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), mwanaharakati huyo mkuu ambaye pia ni mratibu wa Jumuiya ya Wapalestina, alisema kupuuzwa ombi la Kamati ya Olimpiki ya Palestina la kutengwa Israel "kutatia doa pakubwa michezo ya Olimpiki ya Paris na kila mjumbe wa kamati ya Olimpiki."

Katika barua ya wazi kwa mkuu wa IOC Thomas Bach, Shirikisho la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (FIDH) lilitoa wito wa kuchukuliwa hatua za harakati kukabiliana na hali inayozidi kuwa mbaya na kuzorota huko Gaza.

Ikizingatia kigezo kilichowekwa na hatua za IOC dhidi ya Russia na Belarusi FIDH ilisisitiza ulazima wa IOC kuzingatia "ahadi yake ya usawa, haki za binadamu na kutobagua."

Utawala wa Israel umewaua zaidi ya Wapalestina 39,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 90,000 tangu kuanza kwa vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Gaza Oktoba mwaka jana.

Mnamo Januari, Mbunge wa Ufaransa Aymeric Caron aliitaka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kuizuia Israel - kama ilivyofanya kwa Urusi - kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Paris ya 2024 kwa sababu ya vita vya mauaji ya halaiki inayoendesha katika Ukanda wa Gaza. Mwezi Mei, Chama cha Soka cha Palestina (PFA) kiliwasilisha ombi sawa kwa IOC na shirikisho la soka la FIFA, ambalo lilisema kwamba linaahirisha hadi Agosti 31 mjadala rasmi wa ombi la PFA la kusimamisha Shirikisho la Soka la Israeli kimataifa.

3489227

Habari zinazohusiana
captcha